Ibada ya wafu ya msaidizi wa Raila yaandaliwa

  • | KBC Video
    249 views

    Msaidizi wa Raila, marehemu Odinga George Oduor, ametajwa kuwa mtumishi mwaminifu wa chama cha ODM, kinara wa chama na taifa kwa jumla. Wakizungumza wakati wa ibada ya ukumbusho katika kanisa la House of Grace jijini Nairobi, viongozi akiwemo waziri wa kawi Opiyo Wandayi, na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna miongoni mwa wengine, walisema chama hicho kimempoteza mwanachama mwaminifu. Kupitia taarifa iliyosomwa na naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Philip Otieno, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja alisema taifa limempoteza afisa mwenye ujuzi wa hali ya juu wa ulinzi wa watu mashuhuri ambaye alikuwa afisa wa polisi wa kitaifa wa akiba. Oduor atazikwa Jumamosi hii nyumbani kwake kaunti ya Siaya.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive