Idadi kubwa ya wakazi wa Taita Taveta wakosa masomo

  • | Citizen TV
    131 views

    Idadi kubwa ya jamii ya Taita Taveta waliokamilisha masomo yao ya sekondari hushindwa kuendeleza masomo kutokana na umasikini. Viongozi wa kaunti wakikiri kkuwa umekua na changamoto nyingi kufadhili wanafunzi waliohitimu kujiunga na vyuo vya kiufundi na vyuo vikuu.Wakizungumza eneo la taveta ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wengi wa wanafunzi wanasalia kufanya vibarua wanapomaliza elimu ya viwango vya sekondari, viongozi wametaka hatua madhubuti kuchukuliwa ili kusaidia vijana hao kujikwamua kutoka kwa umasikini.