Idadi ya wanafunzi wanaojiunga na shule kaunti ya Kilifi yaongezeka

  • | Citizen TV
    72 views

    Idadi ya watoto wanaojiunga na shule za chekechea katika kaunti ya kilifi imeongezeka kutoka 49,000 hadi 62,000 chini ya miaka miwili. Akiongea katika uzinduzi wa jengo la kisasa la chekechea eneo la Tezo, waziri wa elimu na maswala ya mawasiliano kaunti hiyo Filkin kaingu amedokeza kuwa jengo hilo limewavutia watoto eneo hilo kwa sababu ya mazingira bora. Jengo hilo lina madarasa, ofisi ya walimu, sehemu ya mazoezi kwa watoto, eneo la kupikia,sehemu ya kuhifadhi mizigo pamoja na vyoo vya kisasa .