Idadi ya wavuvi wasiojulikana wauawa katika eneo la Todonyang kaunti ya Turkana

  • | Citizen TV
    889 views

    Idadi isiyojulikana ya wavuvi imeuwawa katika eneo la Todonyang kaunti ya Turkana kufuatia mzozo baina ya jamii mbili kutoka Kenya na Ethiopia. Kwa mujibu wa wakazi, mapigano hayo yalichangiwa na uhasama kuhusu uvuvi ambapo jamii hizo mbili zimekuwa zikizozana kuhusu sehemu ya kuvua samaki katika Ziwa Turkana. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amebaini kuwa serikali inashirikiana na Ethiopia kutafuta suluhu itakayokomesha maafa ya mara kwa mara katika eneo hilo.