Inspekta Jenerali wa polisi akosa kufika mahakamani

  • | Citizen TV
    4,607 views

    Inspekta Jenerali wa polisi Douglas Kanja sasa amepewa makataa ya mwisho kufika mahakamani binafsi tarehe 27 ya mwezi huu, la sivyo akabiliwe na mashtaka ya kudharau mahakama. Hii ni baada ya kukosa kufika mahakama kwa mara ya pili sasa baada ya kuagizwa kufanya hivyo. Kanja alikuwa ameagizwa kufika na kueleza kuhusu ongezeko la utekaji nyara nchini taifa. Hata hivyo, mawakili wake waliomba asamehewe, wakidai kuwa kulikuwa na suala la dharura la kiusalama lililomhitaji kwa haraka wakati alipokuwa akijiandaa kufika mahakamani