Isaac Mutuma kuapishwa kuwa gavana Jumatatu

  • | KBC Video
    1,186 views

    Isaac Mutuma anatazamiwa kuapishwa Jumatatu kuwa gavana wa kaunti ya Meru, baada ya mahakama kuu kudumisha uamuzi wa bunge la Seneti wa kumuondoa madarakani Kawira Mwangaza. Hafla ya kuapishwa kwa Mutuma ambaye kwa sasa ni naibu Gavana wa kaunti hiyo huenda ikatia kikomo kipindi cha kuhudumu cha Kawira kama gavana, ambacho kimekabiliwa na mihemko ya kisiasa. Ripota wetu Abdiaziz Hashim anaangazia masuala ibuka ambayo huenda yataelekeza mustakabali wa kisiasa wa Mwangaza na pia kuangazia safari ya Mutuma ambaye anatazamiwa kuchukua hatamu.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive