Israel kurudia vita Gaza

  • | BBC Swahili
    254 views
    Israel imetishia kufutilia mbali mkataba wa kusitisha vita ikiwa mateka waliopo Gaza hawataachiliwa huru kama ilivyotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii. Katika taarifa iliyotolewa usiku huu, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema jeshi la Israel litarejelea vita ndani ya Gaza, na kuhakikisha kwamba kundi la Hamas limemalizwa kabisa. Hii ni baada ya Hamas kusema kwamba inasimamisha kwa muda usiojulikana, mpango wa kuwarejesha nyumbani mateka wanaozuiliwa Gaza.