Israel na Hezbollah wakijiweka tayari kwa vita kamili iwapo itaanza

  • | VOA Swahili
    113 views
    Katika vijiji vilivyotelekezwa na jamii mbalimbali karibu na mpaka kusini mwa Lebanon, majeshi ya Israeli na wapiganaji wa Hezbollah waliangalia kwa miezi kadhaa, wakihama na kujiweka tayari kwa mapambano wakati wakisubiri kushuhudia vita kamili iwapo vitaanza. Tangu kuanza kwa vita vya Gaza Oktoba mwaka jana, pande hizo mbili zimekuwa zikurushiana wimbi la makombora, roketi, mizinga na mashambulizi ya anga katika mivutano ambayo haijapelekea vita kamili. Maelfu ya watu wamehamishwa kutoka pande zote mbili za mpaka na matumaini kwamba watoto wataweza kurejea kuanza masomo katika mwaka mpya wa masomo ifikapo Septemba inaelekea umekwama kufuatia tangazo la Waziri wa Elimu wa Israel Yoav Kisch Jumanne kuwa hali hivi sasa ilivyo haitaruhusu hilo kufanyika. “Vita inaelekea viko vile vile kwa miezi tisa iliyopita,” Luteni Kanali Dotan, Afisa wa Israeli, ambaye aliweza kutambuliwa kwa jina lake la kwanza. “Tunasiku nzuri za kuishambulia Hezbollah na siku mbaya ambazo wanatushambulia. Ni kama tunalingana kwa hilo, mwaka mzima, miezi yote tisa.” - Reuters #majeshi #israeli #wapiganaji #hezbollah #vita #voa #voaswahili #benjaminnetanyahu #golanheights