Jaji Mkuu Martha Koome asuta nguvu za maafisa

  • | Citizen TV
    7,307 views

    Jaji Mkuu Martha Koome amelaumu hatua ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kuwadhibiti waandamanaji waliokuwa wakipinga mswada tata wa fedha . Koome akisisitiza kuwa wakenya wana haki ya kuandamana kwa amani huku akiahidi kuwa mahakama haitosita kuwapa haki walioathirika na ukiukaji haki wa polisi.