Jamii za Gabra na Daasanach zakubaliana kuzika uhasama baina yao badala yake kuishi kwa amani

  • | KBC Video
    36 views

    Jamii za Gabra na Daasanach zinaoishi sehemu za Dukana na Illeret katika eneobunge la Horr Kaskazini kaunti ya Marsabit zimekubaliana kuzika uhasama baina yao na badala yake kuishi pamoja kwa aman.Akiongea wakati wa mashindano ya siku mbili ya soka katika eneo la Illeret yaliozileta pamoja timu zita za soka kutoka jamii hizo mbili, mwana-harakati wa amani katika jamii ya Daasanach, Mike Kesho alisifia utumizi wa soka kukuza amani na ushirikiano wa kijamii. Mbunge wa Horr Kaskazini, Wario Guyo Adhe ambaye aliongoza mchakato huo wa amani aliwataka wananchi kudumisha amani kwa ajili ya elimu ya watoto wao na utekelezaji miradi katika eneo hilo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive