Jamii za Nyangatom, Toposa na Turkana zaafikia amani

  • | Citizen TV
    101 views

    Jamii ya Nyangatom kutoka Ethiopia,Toposa wa Sudan kusini na Turkana kutoka Kenya ambao tangu jadi wamekuwa wakiishi na uhasama, wamekongamana katika eneo la Koyasa, kaunti ya Turkana kwenye hafla ya kipekee ya kuhimiza amani na maridhiano. Hii ni baada ya serikali kwa ushirikiano na wazee wa jamii hizo kuazimia kuzika uhasama uliopo na kutoa fursa kwa amani katika maeneo ya mpakani.