Jane Wanjiku anawalea watoto eneo la Bamburi

  • | Citizen TV
    216 views

    Aliwacha kazi ya kuwahudumia wanawake na kugeukia kuwalea watoto waliotupwa na mayatima wachanga. Jane Wanjiku Karigoh, mmiliki wa kituo cha watoto cha Calvary Zion eneo la Bamburi kaunti ya Mombasa ameifanya huduma hii akijitolea kwa zaidi ya miaka 25 sasa. Baadhi ya watoto aliowachukuwa wakiwa wametupwa kwenye taka baada ya mama zao kujifungua na amewalea na kuwabadilisha wengine wakiajiriwa na hata kuolewa. Wanjiku ndiye anayetupambia makala ya mwanamke Bomba wiki hii