Je, muungano wa Raila na Ruto utawaridhisha waKenya?

  • | BBC Swahili
    4,964 views
    Rais wa Kenya William Ruto na Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga, wametia saini rasmi mkataba wa kisiasa kufanya kazi pamoja. Mkataba kati ya chama tawala cha Ruto cha United Democratic Alliance (UDA) na Orange Democratic Movement (ODM) cha Odinga umetiwa saini rasmi leo Ijumaa mjini Nairobi. Viongozi wa pande zote mbili walifika katika jumba la KICC kushuhudia kutiwa saini kwa mkataba huo wa makubaliano ambao utahusisha utekelezaji wa masuala kumi. Miongoni mwa masuala hayo ni utekelezaji kamili wa ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Majadiliano (NADCO) ambayo ilitokana na maandamano kufuatia uchaguzi mkuu wa 2022, baada ya Raila kudai kuwa kulikuwa na udanganyifu katika uchaguzi huo. Masuala mengine ni ushirikishwaji wa watu wote katika serikali, uongozi bora, kudhibiti deni la kitaifa, na kupambana na ufisadi. #williamruto #railaodinga #kenya #siasa #bbcswahili #bbcswahilileo