Je, Trump ana jibu la mzozo wa Ukraine, Urusi?

  • | BBC Swahili
    741 views
    Rais wa Marekani Donald Trump amefanya mazungumzo ya simu "ya muda mrefu na yenye tija kubwa" na Rais wa Urusi Vladimir Putin ambapo viongozi hao walikubali kuanza mazungumzo ya kumaliza vita nchini Ukraine. Lakini Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa Kyiv haitakubali makubaliano yoyote ya amani yaliyofikiwa na Urusi na Marekani bila ushiriki wake.