Jiko moja la chakula linawalisha mamia ya wakaazi katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah

  • | VOA Swahili
    182 views
    Jiko moja la chakula linawalisha mamia ya wakaazi katika mji wa kusini mwa Ukanda wa Gaza wa Rafah huku mapigano kati ya Israel na Hamas yakiendelea katika eneo hilo. Jiko hili limekuwa likifanya kazi huku wakazi wengi wa eneo hilo wakiwa wamekwama kwenye eneo la nusu ya kusini mwa Gaza.Huku vivuko vichache vya mpakani vilivyofunguliwa huko Gaza bado kiwango kidogo cha misaada kinafika katika eneo lililozingirwa, ukosefu wa chakula bado ni tatizo kubwa. Umoja wa Mataifa ulisema Jumanne kwamba nusu ya wakazi wa Gaza wako katika hali ya njaa kali na 90% mara kwa mara wanakosa chakula kwa siku nzima. Ni 10% tu ya chakula kinachohitajika kwa watu milioni 2.2 wa eneo hilo kimeingia Gaza katika siku 70 zilizopita, Umoja wa Mataifa ulisema.