Jinsi darasa la densi nchini India linavyosaidia watu wazee kupata furaha

  • | BBC Swahili
    308 views
    Wazee wanaoishi na ugonjwa wa Parkinson nchini India wanasema darasa la densi linawasaidia kuboresha viungo vyao. Mwalimu wao anasema wanafunzi wake katika jimbo la Maharashtra magharibi mwa India wanacheza kwa furaha. Ugonjwa wa Parkinson huathiri jinsi ubongo unavyowasiliana na misuli kwenye mwili. Inaweza kusababisha kutetemeka, kukosa nguvu na kutembea polepole lakini wataalam wanasema mazoezi yanaweza kupunguza kasi ya ugonjwa huo. #bbcswahili #india #parkinson