Jopo la uteuzi wa makamishna wa IEBC laendelea na usaili, awali Erastus Edung Ethekon alisailiwa

  • | TV 47
    60 views

    Jopo la uteuzi wa makamishna wa IEBC laendelea na usaili.

    Leo ni siku ya pili ya mahojiano haya.

    Mwenyekiti wa Jopo ni Nelson Makanda.

    Erastus Edung Ethekon tayari amesailiwa.

    Usaili wa Mwenyekiti kukamilika siku ya Jumatano.

    Watu kumi na mmoja waliteuliwa ili kupigwa msasa katika nafasi ya mwenyekiti.

    Wanaopigwa msasa leo ni Erastus Edung, Francis Kakai Kissinger, Jacob Ngwele Muvengei.

    Aidha Joy Brenda Masinde Mdivo anasailiwa leo.

    Usaili unafanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Bima South C, Nairobi.

    Ili mtu awe Mwenyekiti wa IEBC anahitaji tajriba ya miaka 15 katika sheria.

    Mbali na miaka 15 katika sheria sharti anayeteuliwa kuwa mwenyekiti awe na shahada.

    Usaili wa makamishna utaanza siku ya Alhamisi.

    Ibara ya 88 ya Katiba ya Kenya ndio msingi wa kuwepo kwa IEBC.

    Kazi ya IEBC ni kusajili wapiga kura, kuratibu mipaka na kusimamia uchaguzi.

    Aidha IEBC hutathimini namna vyama vya kisiasa vinavyoendesha mchujo.

    Wanaotaka kuwa Makamishna wa IEBC watasailiwa kuanzia Alhamisi.

    Kuna baadhi ya maeneobunge ambayo hayana wawakilishi bungeni.

    #TV47Matukio @ruga_eval

    Thank you for watching this video. Kindly subscribe for more content from 'Home of The Untold Stories.'

    *About TV47* 'TV47 is on GOtv (Channel 102), DStv (Channel 268), SIGNET, Gotv, BAMBA and STARTIMES. __ For Breaking News, kindly subscribe by sending ‘NEWS’ to 22047. __

    Connect with us:

    Website: https://www.tv47.digital/ Facebook: https://www.facebook.com/TV47KE Twitter: https://twitter.com/tv47news Instagram: https://www.instagram.com/tv47ke/ TikTok: https://www.tiktok.com/@tv47_ke Telegram: https://t.me/tv47_ke WhatsApp: 0797 047 047 __