Juhudi za Qatar kutafuta amani DRC zitafanikiwa?

  • | BBC Swahili
    4,488 views
    Taifa la Qatar limekuwa msitari wa mbele katika juhudi za kutafuta amani kwenye baadhi ya mizozo inayoathiri maeneo kadhaa duniani. Na baada ya kikao cha Jumanne, ambapo Kiongozi wa taifa hilo aliwakutanisha Marais wa Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Qatar imeonekana kuorodheshwa katika kundi la mataifa kama vile Marekani, Milki za Falme za Kiarabu, Saudi Arabia na mengine mengi ambayo yanajaribu kusitisha vita katika bara Ulaya, Mashariki ya kati na hata hapa Afrika. Sasa je, ni kwa nini nchi hiyo imepata umaarufu mkubwa katika juhudi za kusaka amani duniani?. Leila Mohammed anaelezea zaidi. #bbcswahili #qatar #DRC Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw