Kamati ya kuchunguza uuzaji figo hospitali ya Mediheal kuzinduliwa na Waziri Duale

  • | Citizen TV
    120 views

    Kamati mpya ya kuchunguza tuhuma za uuzaji wa viungo nchini imeanza shughuli zake leo, baada ya kuzinduliwa na waziri wa afya Aden Duale. Waziri Aden Duale na maafisa wakuu wa wizara ya afya wameongoza hafla ya uzinduzi wa kamati hii inayoongozwa na Profesa Elizabeth Bukusi. Waziri Duale juma lililopita alibuni kamati hii mpya baada ya kubainika kuwa ripoti ya awali iliyochunguza tuhuma za biashara haramu ya kuuza figo katika hospitali ya Mediheal ilikuwa na dosari.