Kamati ya uteuzi ya bunge yampiga msasa Dorcas Oduor

  • | Citizen TV
    366 views

    Dorcas Agik Oduor, ambaye aliteuliwa kuwa mwanasheria mkuu, hii Leo amefika mbele ya kamati ya bunge inayoendesha zoezi la kuwapiga msasa mawaziri wateule inayoongozwa na spika Moses Wetangula. Oduor ameahidi kuhakikisha kuwa kuna sera mwafaka ya kuongoza jinsi ya kuhusisha umma katika utungaji wa sheria. Iwapo ataidhinishwa, Oduor ataandikisha historia kuwa mwanasheria mkuu wa kwanza wa kike.