Kampeni yafanywa kuimarisha majukumu ya wanaume

  • | Citizen TV
    1,399 views

    Wanaume wametakiwa kuwa kielelezo chema ili kukuza nafasi yao katika jamii. Wito huu umetolewa na viongozi wa kanisa la africa inland (AIC) wanaosema wanaume wametengwa na jamii sehemu nyingi. Viongozi hawa walizungumza haya wakati wa hafla ya kuhitimu kwa wanaume hamsini waliopewa mafunzo maalum ya kuwawezesha kutoa uongozi bora kwa familia na kuwapa vijana wa kiume ushauri unaofaa. Viongozi hao pia wamesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa mafunzo kama hayo ili kuwawezesha wazee na wavulana kuelewa majukumu yao katika jamii.