Kanisa tata lafungwa Rongo

  • | Citizen TV
    1,317 views

    Kizazaa kimeshuhudiwa katika kituo cha Polisi cha Rongo, kaunti ya Migori baada ya waumini zaidi ya 50 kutaka kuishi kanisani licha ya wenzao wawili kufariki. Waumini hao wa kanisa la Melkio St. Joseph Missions of Messaiha walitaka kusalia kanisani na kuendelea kuabudu. Hata hivyo, kamishna wa Migori Mutua Kisilu amesema kanisa hilo lenyewe pia lina utata wa usajili huku ripoti pia zikiarifu kuwa kuna baadhi ya waumini waliopotea.