Katibu Raymond Omolo asema mapendekezo katika ripoti ya Maragaa yameanza kutekelezwa

  • | Citizen TV
    710 views

    Katibu katika wizara ya usalama Raymond Omolo amesema baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa katika ripoti ya jopo kazi la jaji mstaafu David Maraga tayari yametekelezwa ikiwemo nyongeza ya mishahara. Aidha naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amesema kuwa polisi wanaoendeleza ufisadi wamechukuliw ahatua huku idadi ya vizuizi vya barabarani vinavyowekwa na maafisa wa trafiki vikipunguzwa. Haya ni huku mwenyekiti wa tume ya huduma za polisi Eliud Kinuthia akisema kuwa kupelekwa kwa polisi Haiti kumepunguza idadi ya maafisa wa polisi nchini.