Kaunti ya Kilifi yasisitiza ina dawa za kutosha

  • | KBC Video
    7 views

    Serikali ya kaunti ya Kilifi imekanusha madai ya kuwepo kwa uhaba wa dawa katika taasisi za afya za umma. Akiongea wakati wa ziara katika zahanati ya Palakumi, afisa mkuu anayesimamia zahanati katika kaunti ya Kilifi, Edward Mumbo alisema kuwa zahanati-142 hupokea dawa kila wakati na kwamba uchunguzi hufanywa kuhakikisha wakazi wanafurahia huduma bora za matibabu.Hatua hii imejiri siku kadhaa baada ya baadhi ya wakazi wa Kilifi kuandamana katika kaunti ya zahanati ya Palakumi wakilalamikia huduma duni za matibabu katika zahanati hiyo. Zahanati ya Palakumi ni kituo muhimu cha afya kinachodumia zaidi ya familia elf-1 kutoka maeneo ya Ganze na Kaloleni.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive