KeNHA yafungua barabara ya Southern Bypass

  • | KBC Video
    72 views

    Halmashauri ya kitaifa ya kusimamia barabara kuu-KeNHA imefungua tena sehemu ya barabara ya pembezoni mwa jiji la Nairobi iliyokuwa imefungwa tarehe 24 mwezi uliopita kwa ajili ya ukarabati. ; Akizungumza wakati wa ufunguzi wa sehemu ya barabara, naibu mkurugenzi wa mawasiliano ya umma katika halmashauri ya KeNHA, Samuel Kumba alisema ukarabati huo ulihusisha uwekaji vishikizi kwenye sehemu tatu zikiwemo daraja la Ole Sereni, barabara ya juu kwa juu ya Kibera na barabara ya Ngong baada ya kugundua kwamba vishikizi vya awali vimelegea. Aliongeza kuwa halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto ya kuweka taa za barabarani ili kuzuia visa vya utovu wa usalama.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive