Kenya kuwapeleka polisi 600 Haiti kurejesha utulivu

  • | KBC Video
    44 views

    Kenya itawapelaka maafisa 600 zaidi wa polisi,kujiunga na kikosi cha kimataifa cha kudumisha amani nchini Haiti.Rais William Ruto amesema maafisa hao wa ziada wanatarajiwa kuungana na wenzao 400,ambao tayari wamo katika taifa hilo la Carribean,jamii ya kimataifa ikifanya juhudi kurejesha amani na uthabiti nchini humo.Rais Ruto ambaye alishauriana na waziri mkuu wa Garry Connile ambaye yuko humu nchini kwa ziara rasmi ya siku nne,wakati uo huo ameihimiza jamii ya kimataifa kutimiza ahadi yake kuhusiana na ufadhili wa kikosi hicho,akitahadharisha kuwa juhudi hizo zinaweza kulemazwa kutokana na uhaba wa maafisa,vifaa na fedha.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News