Kenya yalalamika kuhusu Tanzania kutoa vibali kwa michezo ya shabaha

  • | VOA Swahili
    136 views
    Tanzania na Kenya nchi majirani Afrika Mashariki kila mmoja anasimamia makundi ya tembo kwa njia tofauti. Kenya ina msimamo wa kutovumilia kabisa uwindaji wa wanyama pori na uuzaji wa pembe za ndovu huku ikipata mapato yake kwa watalii wanaokuja nchini kutazama wanyama hao. Lakini Tanzania inatoa leseni za uwindaji kwa wanaofanya hivyo kama michezo ya kulenga shabaha kila mwaka. Je, wito wa Kenya kuitaka Tanzania kuwawekea wawindaji wake mipaka kama njia ya kuwalinda Tembo wa Kenya itafaulu? Ungana na mwandishi wetu akukuletea ripoti kamili kuhusu kadhia hiyo. Endelea kusikiliza... #tanzania #kenya #tembo #uwindaji #utalii #afrikamashariki #pembe #ndovu #mapato #uwindaji #shabaha #wito #michezo #voa #voaswahili