Kenya yalaumiwa kwa mzozo wa Sudan

  • | BBC Swahili
    933 views
    Sudan imeikosoa vikali Kenya kwa kuwa mwenyeji wa utiaji saini wa mkataba wa kisiasa kati ya wanamgambo wa RSF na washirika wao. Mkataba unaotarajiwa kutiwa saini hapo Ijumaa unalenga kuunda serikali mbadala katika maeneo ya Sudan yanayodhibitiwa na RSF. Hata hivyo, Kenya imesisitiza kwamba ina historia ya kusimamia mazungumzo ya kusuluhisha mizozo kati ya pande hasimu kwenye mataifa jirani. Aidha Waziri wa Mambo ya Kigeni Musalia Mudavadi amesema kwamba Kenya inaunga mkono mkutano unaoendelea Nairobi ikiwa kama msuluhishi asiye egemea upande wowote.