Kesi ya DRC dhidi ya Rwanda yaanza kusikilizwa Arusha, Tanzania

  • | BBC Swahili
    111 views
    Kesi iliyofunguliwa na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Afrika ya haki za watu na zile za Binadamu imeanza kusikilizwa jijini Arusha, Tanzania Kesi hiyo inayosikilizwa kwa siku mbili Februari 12 na 13 inahusu mapigano ya tangu Mwaka 2021, kati ya vikosi vya Kongo na waasi wa M23 ambao Kongo inadai wamekuwa wakifadhiliwa na Rwanda. Je Kongo inaishitaki Rwanda kwa madai yapi? @sammyawami anaelezea zaidi #bbcswahili #tanzania #DRC Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw