Kesi za Ardhi Kwale

  • | Citizen TV
    330 views

    Mahakama ya Kwale imewarai wakaazi kusuluhisha kesi nje ya mahakama ili kuzuia mrundiko wa kesi mahakamani. Jaji wa mahakama ya mazingira na ardhi Lucas Naikuni amesmea kesi nyingi za ardhi zinaweza kusuluhishwa kwa haraka nje ya mahakama na kuepukana na mahangaiko ya kusibiri kesi kutatuliwa mahakamani kwa muda mrefu. Kwa sasa zaidi ya kesi 4,000 za ardhi hazijatatuliwa Kwale kutoka mwaka wa 2016. Lawrence Ng'ang'a anaarifu zaidi kutoka Kwale.