Kielelezo cha bajeti kufanyiwa marekebisho

  • | KBC Video
    29 views

    Kundi la wabunge wa mrego wa Kenya Kwanza limewahakikishia Wakenya kuwa rasimu ya bajeti ya kitaifa iliyopendekezwa siyo ya mwisho kwani wananuia kuifanyia marekebisho makubwa bungeni. Wakiongozwa na mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri, viongozi hao walisema watapatia suala la ulipaji wa madeni ya serikali kipaumbele ili kuhakikisha uendelevu wa kifedha wa taifa hili mbali na kukamilishwa kwa miradi muhimu ya maendeleo kabla ya kuzinduliwa kwa mingine mipya. Viongozi hao waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa maktaba katika shule ya msingi ya Kanjeru walikariri kujitolea kwao kuunga mkono mipango ya serikali wakisema kufanya hivyo kuna manufaa mengi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive