Kikundi cha marafiki wa msitu wa Karura wakanusha madai ukataji miti

  • | K24 Video
    21 views

    Kikundi cha marafiki wa msitu wa Karura, ambacho hujitolea kutunza na kulinda msitu huo, kimedai kwamba ukataji miti unaoendelea unahusisha kukata miti isiyo ya asili kama saru, mkalatusi, na kupanda miti ya asili kama vile mwoki mweupe. Mwenyekiti wa kikundi hicho, profesa Karanja Njoroge, anasema mpango huo umekuwa ukitekelezwa tangu mwaka wa 2010, ambapo waliondoa miti ya zamani na kupanda miti mipya katika eneo lenye ukubwa wa ekari kumi, amewapa wakenya hakikisho kuwa ardhi hiyo hainyakuliwi kama inavyodaiwa katika mitandao ya kijamii.