Kilimo Biashara | Kilimo cha Pamba ya BT

  • | Citizen TV
    242 views

    Kilimo cha pamba ya BT kimeleta manufaa mengi na kuboresha mazingira ya baharini katika kaunti ya Lamu. Kwa miaka mingi, kemikali zinazotumiwa katika kilimo cha kawaida cha pamba zimekuwa zikichafua maji ya bahari na kutishia maisha ya viumbe vya baharini kama vile samaki. Hali hiyo imechangia kupungua kwa idadi ya wanyama wa baharini. Lakini sasa, kupitia kilimo cha pamba ya kısasa ya BT, wakulima wameweza kuboresha mazao na kujinufaisha kando na kuimarisha mazingira.