Kilio cha fidia Kajiado

  • | Citizen TV
    517 views

    Waathiriwa wa mashambaulizi ya wanyamapori katika kaunti ya Kajiado wanalalamikia kucheleweshwa kwa fidia baada ya kushambuliwa na wanyama hao. wakazi hao wanasema kuwa serikali imepuuza suala la fidia ilhali baadhi wamepoteza wapendwa ao huku wengine wakisalia na majeraha. wakazi hao wameieleza kamati inayochunguza athari za migogoro baina ya wakazi na wanyamapori kuwa baadhi yao wamesubiri fidia tangu mwaka wa 2014.