Kisunzi cha Ajira Nchini: Takwimu za KNBS zasema watu milioni tisa hawajapata ajira

  • | Citizen TV
    248 views

    Kulingana na ripoti ya shirika la takwimu za kitaifa nchini, idadi ya watu wanaotafuta ajira imekuwa ikiongezeka lakini nafasi za ajira zinapungua kila uchao. Kwenye ripoti hiyo ya KNBS, watu zaidi ya milioni tisa wa kati wa hadi miaka 64 hawajapata ajira kwa muda mrefu. Nalo shirikisho la waajiri nchini FKE limetabiri kuwa mazingira mabaya ya kiuchumi yatazisukumu kampuni zaidi kushindwa kumudu biashara na hivyo kuwafuta kazi wafanyikazi zaidi.