Kituo cha utafiti wa ubaharia cha Kabonyo Kanyagwal kukamilika mwaka ujao

  • | Citizen TV
    90 views

    STBY VCR NATS UP Mradi wa eneo la utafiti wa ubaharia wa Kabonyo Kanyagwal utakamilika kufikia mwezi Juni mwaka ujao, ili kuimarisha shughuli za uvuvi katika ukanda wa Magharibi Akizungumza baada ya kuzuru mradi huo eneo la Nyando kaunti ya Kisumu, naibu rais Kithure Kindiki alisema kuwa ujenzi huo ni mojawapo ya miradi ya kupiga jeki uchumi wa majini humu nchini ili kubuni nafasi zaidi za ajira. Vile vile mradi huo unatarajiwa kutoa maji ya unyunyuzaji ili kukuza kilimo katika kaunti ya Kisumu. Rais William Ruto alizindua mradi wa Kabonyo Kanyagwal mwaka 2023 na unatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 1.3 kujenga kituo cha utafiti na uzalishaji wa samaki.