Kiwanda cha uchakataji wa asali Tanzania

  • | BBC Swahili
    449 views
    Ufugaji wa nyuki ni moja ya sekta inayotegemewa na jamii nyingi pamoja na serikali katika kuingiza kipato hasa katika ukanda wa magharibi mwa Tanzania huku changamoto kubwa ilikuwa ni upatikanaji wa soko la uhakika. Lakini huenda sasa changamoto hii ikabaki historia baada ya kuanzishwa kiwanda cha uchakataji wa asali na kusafirishwa kwenda katika masoko ya nje. Mwandishi wetu Alfred Lasteck katembelea kiwanda hicho cha Upendo Honey na kuandaa taarifa hii… #bbcswahili #tanzania #kigoma