Kizaazaa mjini Busia baada ya mwanaume kumfumania mkewe na mpango wa kando chumbani

  • | Citizen TV
    8,458 views

    Kizaazaa kilizuka huku shughuli za kawaida zikisitishwa kwa muda mjini Busia baada ya mwanamme mmoja kuandamana na mlolongo wa wa wahudumu wa bodaboda akilalamikia kunyang'ang'anywa mkewe. Mwanaume huyo kwa jina Philip Munala kutoka mtaa wa Mauko viungani mwa mji wa Busia anasema kuwa amekuwa na mzozo na mkewe kabla yake kumfumania katika uhusiano mwingine.