Kliniki 150 zafungwa baada ya marekani ilisitisha ufadhili kupitia shirika la USAID

  • | Citizen TV
    287 views

    Mashirika yasiyo ya serikali sasa yanasema kuwa hatua ya Marekani kuondoa ufadhili kupitia shirika la USAID umezidi kubana huku wafanyakazi elfu 35 wakiwa hawana kazi. Aidha, mashirika haya pia yanasema zaidi ya kliniki mia moja zimefungwa tayari nchini. Wadau hawa wa sekta ya afya haswa wale wanaoshughulikia UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu sasa wakiitaka serikali kuweka juhudi kurejesha huduma za matibabu ya magonjwa hayo