KNUT yapinga madai ya mwalimu mmoja wa JSS kupigwa na mwalimu mkuu Nyamira

  • | Citizen TV
    711 views

    Chama cha walimu wa shule za msingi nchini KNUT tawi la Nyamira kimepinga madai ya mwalimu mmoja wa JSS kupigwa na mwalimu mkuu katika shule ya msingi ya Nyanchoka HUKO Mugirango kaskazini katika kaunti ya Nyamira, na kusema ni njama ya kumharibia jina mwalimu mkuu wa shule hiyo.katibu mkuu wa KNUT Nyamira Evans Obiri amesema wamefanya uchunguzi wao, na kubaini kwamba mwalimu huyo hakupigwa anavyodai.