Kongamano la COP29 laendelea Azerbaijan

  • | KBC Video
    1 views

    Ulimwengu huenda ukakosa kutimiza lengo la kimataifa la kuongeza maradufu matumizi bora ya nishati ifikapo mwaka 2030, kuambatana na mwafaka uliopitishwa katika kongamano la COP 28 lililoandaliwa katika Muungano wa Milki za Kiarabu. Haya yamesemwa na wafanyabiashara na mashirika yanayohudhuria kongamano la COP 29 huko Baku, Azerbaijan. Haya yanajiri huku maelfu ya wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi wakiandamana mjini Baku kushinikiza mataifa yaliyostawi kutuma ruzuku zaidi kwa mataifa ambayo hayajaendelea na ambayo bado yanakabiliwa na athari nyingi za mabadiliko ya hali ya hewa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive