Kuachiliwa kwa Stephen Munyakho

  • | Citizen TV
    103 views

    Baraka kuu la waislamu nchini supkem limewapongeza wahisani waliotoa mchango wa fidia ili kumuokoa mkenya Stephen Munyakho aliyehukumiwa kifo nchini Saudi Arabia. Munyakho alishtakiwa kwa mauaji na hivyo familia ya mwathiriwa ikadai fidia ya shilingi milioni 150 la sivyo anyongwe. Hata hivyo, jukwaa la waislamu duniani lilitoa mchango wa dola milioni moja kumkomboa munyakho ambaye anatarajiwa kurejea humu nchini hivi karibuni.