Kulinganisha gharama za uchaguzi wa Marekani na zile za nchi nyingine

  • | VOA Swahili
    122 views
    Uchaguzi wa Marekani ni miongoni mwa chaguzi zenye gharama kubwa zaidi duniani. Uchaguzi mkuu wa Uingereza mwaka 2019, matumizi ya kisiasa yalikuwa mara 24 chini kuliko ya uchaguzi wa Marekani 2020. Wakati wa uchaguzi wa Australia mwaka 2019, vyama vya siasa vilitumia chini ya nusu ya vyama vya siasa vya Marekani vilivyotumia kwa kila mtu mwaka uliofuata. India kihistoria ilikuwa na uchaguzi wa gharama sana mwaka 2019. Kiwango hicho kilizidi matumizi ya wakati wa uchaguzi wa Marekani mwaka 2016, lakini hakikufikia gharama za uchaguzi wa Marekani 2020. Mwaka 2020, zaidi ya dola bilioni16 zilitumika katika uchaguzi wa rais na wabunge. Hiyo inajumuisha pesa zote zilizotumiwa na wagombea urais, wagombea wa seneti na wawakilishi, vyama vya siasa na makundi huru yanajaribu kufanya ushawishi katika uchaguzi. Wagombea wanatumia pesa kwenye nini? Kiwango kikubwa kinakwenda kwenye matangazo. Aina nyingine za matumizi ni pamoja na gharama za uendeshaji, mishahara ya wafanyakazi wa kampeni, na jitihada za uchangishaji pesa ili kupata pesa zaidi. Je, mgombea tajiri sana anaweza kushinda? Si wakati wote, lakini mara nyingi. Wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula Marekani wa 2022, asilimia 93 ya wagombea katika baraza la wawakilishi walitumia pesa nyingi zaidi na asilimia 82 ya wagombea waliotumia peza nyingi katika seneti walishinda. Mara baada ya mgombea kushinda uchaguzi, utegemezi wa pesa hauishi. Maafisa waliochaguliwa mara kwa mara hutumia sehemu ya siku zao kuchangisha pesa kwa ajili ya kampeni ijayo. #uchaguzimarekani2024 #gharama #matumizi #seneti #wawakilishi #voa #voaswahili #warepublikan #wademokratiki #dunia