Kundi la vijana wavamia wakaazi wa Diani na kuwashambulia kwa mapanga kabla ya kuwapora

  • | Citizen TV
    4,260 views

    Hali ya taharuki ingali imetanda katika kaunti ya Kwale baada ya kundi la vijana kuvamia wakazi wa eneo la Diani na kuwashambulia kwa mapanga kabla ya kuwapora. Inaarifiwa kuwa vijana hao maarufu “Panga Boys” walijitokeza wakidai kuandamana kufuatia kifo cha mwanaume mwenye umri wa miaka 29 aliyedungwa kisu Ijumaa, ila wakatumia fursa hiyo kuwahangaisha na kuwapora wakazi wa eneo hilo.