Kundi la wapiganaji wa Sudan, RSF launda muungano wa kisiasa jijini Nairobi

  • | Citizen TV
    3,979 views

    Kundi la wapiganaji wa Sudan RSF pamoja na vyama vya kisiasa 20 na asasi tofauti za kiraia nchini Sudan zimetia saini makubaliano ya kuunda muungano mpya wa kisiasa. Muungano huo wa uanzilishi wa Sudan unalenga kutoa uongozi wa taifa hilo liliokumbwa na vita dhidi ya RSF na Jeshi la Sudan SAF. Kuundwa kwa Muungano huo jijini Nairobi kunajiri wakati ambapo kumekuwa na masuali mengi kuhusu Kenya Kuunga mkono Kundi hilo la wanamgambo.