Kwa nini kimbunga hatari kilichoikumba Afrika kimevunja rekodi?

  • | BBC Swahili
    1,058 views
    Kimbunga cha kitropiki Freddy kimeikumba pwani ya kusini mwa Afrika na kuua takriban watu 225 katika nchi za Malawi, Msumbiji na Madagascar, na kufanya watu takriban 25,000 kuyahama makazi yao. Dhoruba hii imevunja angalau rekodi moja - kimbunga kinachokusanya nguvu zaidi (ACE), kipimo kinachozingatia nguvu za upepo wa dhoruba. Kulingana na Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa Ulimwenguni, kimekusanya nguvu sawa na msimu mzima wa vimbunga vya Atlantiki ya Kaskazini, na inaweza kuendelea kuvunja rekodi zaidi. Kadiri mabadiliko ya hali ya hewa yanavyosababisha joto baharini, nguvu ya joto kutoka kwenye uso wa maji inachochea dhoruba kali zaidi. #bbcswahili #kimbungafreddy #malawi