Kwa nini serikali ya DRC iko tayari kuzungumza na M23?

  • | BBC Swahili
    3,429 views
    Baada ya kikao na Rais Felix Tsishekedi wa DRC jijini Luanda, Rais wa Angola anasema kwamba taifa lake litajaribu kibinafsi kupanga mkutano kati ya serikali ya DRC na kundi la waasi la M23 katika siku chache zijazo. M23 ni mojawapo ya karibu makundi 100 yenye silaha yaliyopo katika eneo lenye utajiri wa madini la mashariki mwa DRC. Katika mashambulizi ya tangu Januari mwaka huu, M23 imedhibiti maeneo kadhaa mashariki mwa Congo, ikiwemo miji ya Goma na Bukavu.