M23 waandaa mkutano Goma

  • | BBC Swahili
    9,609 views
    Kundi la waasi la M23 limeandaa mkutano wa kisiasa katika mji wa Goma waliouteka wiki jana. Umati mkubwa wa watu ulihudhuria mkutano huo wa hadhara na kufunga barabara zote zinazoelekea kwenye uwanja wa michezo wa Unity. Wakuu wa kundi hilo walihutubia mkutano huo, siku moja tu baada ya kutangaza serikali mpya ya jimbo la Kivu Kaskazini. Pia kumekuwa na mkutano mkubwa wa kanisa jijini Kinshasa unaolenga kutafuta suluhu la kidiplomasia na kisiasa kwenye mzozo wa mashariki mwa Congo.