Maaandalizi ya mazishi katika Hospitali ya AL-Aqsa Martyrs

  • | VOA Swahili
    492 views
    Mashambulizi ya angani yaliyofanywa na Israeli Jumanne yameuwa Wapalestina wasiopungua 17 katika kambi mbili zilizo kuwa za kwanza kuanzishwa katika Ukanda wa Gaza na vifaru vya Israeli viliingia ndani zaidi ya eneo finyu la mji wa Rafah ulioko kusini, wakazi na wafanyakazi afya walisema. Maandalizi ya Mazishi yakiendelea katika Hospitali ya AL-Aqsa Martyrs huko Deir AL-Balah, Gaza, ambapo familia kadhaa zilipoteza wapendwa wao katika mashambulizi ya angani yaliofanywa na Israeli. Wakazi wameripoti mashambulizi ya mabomu yenye nguvu yanayofanywa na vifaru na ndege kadhaa katika maeneo kadhaa ya Rafah, ambapo zaidi ya watu milioni moja walikuwa wamekimbilia kutafuta hifadhi kabla ya mwezi Mei. Wengi kati ya watu hao wamekimbilia kaskazini tangu wakati huo wakati majeshi ya Israeli yalipokuwa yakivamia mji huo. Tangu Hamas ilipofanya shambulizi Oktoba 7, mashambulizi ya Israel huko Gaza yameuwa zaidi ya Wapalestina 37,400, kulingana na maafisa wa afya wa Gaza. Hamas inayoongozwa na watu wenye silaha imeua takriban watu 1,200 na kuwateka watu zaidi ya 250 katika uvamizi wa Oktoba 7 waliofanya ndani ya Israel, kulingana na hesabu iliyojumlishwa na Israel. -Reuters #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #kufrdan #jenin #wanamgambo #wapalestina #jeshi #israel #Deiralbalah