Maadhimisho ya mwezi wa hamasisho la saratani ya matiti

  • | K24 Video
    9 views

    Huku dunia ikiadhimisha mwezi wa hamasisho la saratani ya matiti, wagonjwa wa saratani na waliopona wametoa wito kwa serikali, kuweka rasilimali za kutosha katika kupigana na janga la saratani. Wadau hao wanaitaka serikali iboreshe matibabu ya saratani na kurahisisha kupatikana kwake. Waziri wa afya dkt Deborah Mulongo aliyekuwa mgeni wa heshima katika uwanja wa bumula katika kaunti ya Bungoma, amesema serikali imeweka mikakati ya kutosha kwa minajili ya matibabu ya wagonjwa wa saratani kupitia bima mpya ya afya ya SHIF